Jumatatu, 10 Aprili 2023

MUACHE KUNIA BUDU MIMI SIO YESU

ROBERT POWELL MUIGIZAJI WA FILAMU YA YESU AMEWAAMBIA WAKRISTO   "MIMI SIYO YESU, ACHENI KUNIABUDU"

 Mwigizaji Robert Powell, mtu aliyeigiza uhusika wa"Yesu" katika filamu maarufu ya Yesu wa Nazareti amewasihi wanaoabudu Picha yake wakiamini kuwa yeye ndiye Yesu waache.

 anasema “ACHENI KUNIABUDU MIMI SIYO YESU”

 Tangu Robert alipoigiza uhusika wa Yesu katika filamu ya mwaka 1977, Jesus of Nazareth, picha za Robert Powell zimetundikwa makanisani, majumbani, kwenye magari, mashuleni, maofisini na kwenye majumba mengi matakatifu duniani kote wakiamini kuwa yeye ndiye Yesu wa Nazareth.

 Hata hivyo, Powell amepiga kelele kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye si Yesu na watu waache kumwabudu.  Badala yake, wanapaswa kumstahi Yesu wa kweli na kumwabudu Mungu.

 Kwa maneno yake aliandika: “Siachi kusema na ninarudia kwa ulimwengu tangu 1977. Mimi sio Yesu Kristo, mimi ni mwigizaji wa kawaida tu kutoka Uingereza.  Nimechoka kuona picha zangu zikiwa katika sehemu za ibada"

" Ninatengeneza filamu ili kujipatia riziki.  Choma picha yangu na kumwabudu Mungu pekee katika ukweli!  Mimi ni mwigizaji tu ... Yesu ni Bwana!

Follow 👉 mapambo Xclussive Media on Facebook and Instagram

Jumamosi, 8 Aprili 2023

Mvuvi aipata kamera iliyozama majini 2010 ikiwa na memori kadi ndani yake ambayo haijaharibika...Baada ya miaka 13 ndani ya maji, kamera hiyo ilipatikana imechakaa na kujaa maji ndani lakini memori kadi ilikuwa vizuri hadi kusoma kwenye kompyuta.Muhtasari• Wiki iliyopita, hata hivyo, mvuvi wa kuvua samaki alikuwa akifanya uvuvi kwenye mto na kugundua kitu cha kushangaza.• Hazina ambazo Greiner alipata zilikuwa picha za safari ya Amayi, pamoja na sherehe ya harusi ya rafiki.• Wiki iliyopita, hata hivyo, mvuvi wa kuvua samaki alikuwa akifanya uvuvi kwenye mto na kugundua kitu cha kushangaza.• Hazina ambazo Greiner alipata zilikuwa picha za safari ya Amayi, pamoja na sherehe ya harusi ya rafiki.Memori Kadi yapatikana ikiwa sawa ndani ya kamera iliyozama majini miaka 13 iliyopita.Mwanamke anatarajiwa kuunganishwa tena na kamera yake ya kidijitali, miaka 13 baada ya kudhani kuwa hangeipoteza milele katika mto Colorado.Coral Amayi alikuwa na picha za harusi ya marafiki zake na kuhitimu kwake mwenyewe kati ya kumbukumbu zingine za kupendeza kwenye kamera ya kidijitali ya Olympus na alipoteza kwa bahati mbaya kwenye Mto Animas mnamo 2010."Nilikuwa nimerushwa kutoka kwa mtumbwi wangu huko Smelter Rapid," alisema. 'Na nilirudi, nikachukua mtumbwi, na kamera yangu haikuwepo.'’ Fox News waliripoti.Wiki iliyopita, hata hivyo, mvuvi wa kuvua samaki alikuwa akifanya uvuvi kwenye mto na kugundua kitu cha kushangaza.Spencer Greiner alitazama kwenye maji ya kina kifupi na hakuwa na uhakika kabisa amepata nini."Nilikuwa nikitembea na kuiona ikitoka kwenye mchanga," Spencer Greiner aliiambia Fox 31.

Niliomba na kufunga nipate mume, nikakutana naye wiki moja baadaye- Mercy Masika Alisema alijua David angekuwa mumewe punde baada ya kukutana naye mara ya kwanza.Muhtasari•Masika alifichua kwamba alikutana na mume wake David Muguro na kuchumbiana naye baada ya kukamilisha masomo yake ya chuo kikuu.•"Nilikuwa na nia ya maombi yangu. Tulifunga ndoa, ilikuwa nzuri na sasa tuna watoto watatu. Tuko hapa sasa," alisema.•Masika alifichua kwamba alikutana na mume wake David Muguro na kuchumbiana naye baada ya kukamilisha masomo yake ya chuo kikuu.•"Nilikuwa na nia ya maombi yangu. Tulifunga ndoa, ilikuwa nzuri na sasa tuna watoto watatu. Tuko hapa sasa," alisema.Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili, Mercy Masika amefunguka kuhusu ndoa yake ya takriban mwongo mmoja unusu.Akizungumza kwenye mahojiano na Citizen TV, mama huyo wa watoto watatu alifichua kwamba alikutana na mume wake David Muguro na kuchumbiana naye baada ya kukamilisha masomo yake ya chuo kikuu.Alifichua kuwa mkutano wake wa kimiujiza na Bw David ulikuja wiki moja tu baada ya kusali na kufunga ili kupata mume."Ilikuwa Januari, nilikwenda kuomba, nilifunga siku tano hivi, nikasema 'Mungu, nimechumbiana na watu wengi sana hasa watumishi', nikasema 'Mungu hata sitaki mchungaji, naomba nionyeshe huyo mtu. Cha kushangaza, tulikutana wiki iliyofuata," Masika alisema.Mwimbaji huyo wa kibao 'Mwema' alisema kwamba mkutano wa kwanza na mumewe ilikuwa ya kawaida tu. Wawili hao waliendelea kuchumbiana kwa miezi kadhaa kabla ya kufunga pingu za maisha hatimaye."Nilikuwa na nia ya maombi yangu. Tulifunga ndoa, ilikuwa nzuri na sasa tuna watoto watatu. Tuko hapa sasa," alisema.Masika alisema walichumbiana sana na mumewe na kuzungumza mengi kabla ya kuchukua hatua ya kufanya harusi. Alibainisha kuwa maisha yake ya maombi yamechangia pakubwa kufanikisha ndoa yake.Mwanamuziki huyo alifichua kwamba alipata mpenzi wake wa kwanza akiwa katika chuo kikuu cha Daystar ila mahusiano hayo hayakudumu."Alikuwa mtu mcha Mungu sana. Alikuwa akinifundisha neno la Mungu. Lakini haikufanya kazi," alisema.Aliendelea kujaribu mahusiano na wacha Mungu wengine katika chuo kikuu ila hakuna ambayo yalidumu. Alisema hatimaye alikutana na Bw David mwaka ambao alikuwa akihitimu na wakafunga ndoa mwaka moja baadaye.Katika mahojiano ya awali, Masika alifichua kwamba alikutana na mwenzi wake wa maisha alipokuwa akitumbuiza kwenye karamu ya harusi katika eneo la Lang'ata ambapo Muguro alikuwa mpiga video."Aliomba nambari yangu baada ya tukio akipendekeza kwamba angependa niimbe kwenye harusi yake siku moja," alisema.Alisema alijua David angekuwa mumewe punde baada ya kukutana naye mara ya kwanza.

MTOTO Eliud Jarome (2) ameuawa baada ya kushambuliwa na fisi akiwa na watoto wenzake wakitafuta kuni katika Kata ya Zugimlole Tarafa na Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora.-Akizungumza na vyombo vya habari jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao alisema kwamba tukio hilo lilitokea Aprili 5, mwaka huu.-Alisema kwamba kwa kuwa mtoto huyo alikuwa mdogo hakuweza kukimbia na hivyo kushambuliwa na fisi.-Kamanda Abwao alisema kwamba askari wa wanyamapori walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumuua fisi huyo.-Wakati huo huo polisi mkoani humo imewataka wananchi kuelekea kwenye ibada na sherehe za Sikukuu ya Pasaka washerehekee kwa amani na utulivu kwa kufuata sheria za nchi.-Kamanda Abwao aliwataka madereva wa vyombo vya moto wajiepushe na mwendo kasi, kupita magari mengine sehemu hatarishi na kutumia kilevi cha aina yoyote wakati wakiendesha vyombo vya moto.-Aliwataka pia wananchi kuendelea kushirikiana na polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu ili kuendelea kuuweka mkoa katika hali ya usalama.-#DirayaUlimwengu#mapambopodcast#mapamboupdateshttps://www.facebook.com/100071151501467/posts/pfbid0FSmjwU9W2yVfpzc959SWLjaU2taXr46x1zPrZe4UhUYSuhr1jacffVEaGDNAusSZl/?app=fbl

MUACHE KUNIA BUDU MIMI SIO YESU

ROBERT POWELL MUIGIZAJI WA FILAMU YA YESU AMEWAAMBIA WAKRISTO   "MIMI SIYO YESU, ACHENI KUNIABUDU"  Mwigizaji Robert P...