Jumamosi, 8 Aprili 2023
MTOTO Eliud Jarome (2) ameuawa baada ya kushambuliwa na fisi akiwa na watoto wenzake wakitafuta kuni katika Kata ya Zugimlole Tarafa na Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora.-Akizungumza na vyombo vya habari jana ofisini kwake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Richard Abwao alisema kwamba tukio hilo lilitokea Aprili 5, mwaka huu.-Alisema kwamba kwa kuwa mtoto huyo alikuwa mdogo hakuweza kukimbia na hivyo kushambuliwa na fisi.-Kamanda Abwao alisema kwamba askari wa wanyamapori walifika eneo la tukio na kufanikiwa kumuua fisi huyo.-Wakati huo huo polisi mkoani humo imewataka wananchi kuelekea kwenye ibada na sherehe za Sikukuu ya Pasaka washerehekee kwa amani na utulivu kwa kufuata sheria za nchi.-Kamanda Abwao aliwataka madereva wa vyombo vya moto wajiepushe na mwendo kasi, kupita magari mengine sehemu hatarishi na kutumia kilevi cha aina yoyote wakati wakiendesha vyombo vya moto.-Aliwataka pia wananchi kuendelea kushirikiana na polisi kwa kutoa taarifa za wahalifu ili kuendelea kuuweka mkoa katika hali ya usalama.-#DirayaUlimwengu#mapambopodcast#mapamboupdateshttps://www.facebook.com/100071151501467/posts/pfbid0FSmjwU9W2yVfpzc959SWLjaU2taXr46x1zPrZe4UhUYSuhr1jacffVEaGDNAusSZl/?app=fbl
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
MUACHE KUNIA BUDU MIMI SIO YESU
ROBERT POWELL MUIGIZAJI WA FILAMU YA YESU AMEWAAMBIA WAKRISTO "MIMI SIYO YESU, ACHENI KUNIABUDU" Mwigizaji Robert P...
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni