Jumamosi, 8 Aprili 2023

Niliomba na kufunga nipate mume, nikakutana naye wiki moja baadaye- Mercy Masika Alisema alijua David angekuwa mumewe punde baada ya kukutana naye mara ya kwanza.Muhtasari•Masika alifichua kwamba alikutana na mume wake David Muguro na kuchumbiana naye baada ya kukamilisha masomo yake ya chuo kikuu.•"Nilikuwa na nia ya maombi yangu. Tulifunga ndoa, ilikuwa nzuri na sasa tuna watoto watatu. Tuko hapa sasa," alisema.•Masika alifichua kwamba alikutana na mume wake David Muguro na kuchumbiana naye baada ya kukamilisha masomo yake ya chuo kikuu.•"Nilikuwa na nia ya maombi yangu. Tulifunga ndoa, ilikuwa nzuri na sasa tuna watoto watatu. Tuko hapa sasa," alisema.Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Injili, Mercy Masika amefunguka kuhusu ndoa yake ya takriban mwongo mmoja unusu.Akizungumza kwenye mahojiano na Citizen TV, mama huyo wa watoto watatu alifichua kwamba alikutana na mume wake David Muguro na kuchumbiana naye baada ya kukamilisha masomo yake ya chuo kikuu.Alifichua kuwa mkutano wake wa kimiujiza na Bw David ulikuja wiki moja tu baada ya kusali na kufunga ili kupata mume."Ilikuwa Januari, nilikwenda kuomba, nilifunga siku tano hivi, nikasema 'Mungu, nimechumbiana na watu wengi sana hasa watumishi', nikasema 'Mungu hata sitaki mchungaji, naomba nionyeshe huyo mtu. Cha kushangaza, tulikutana wiki iliyofuata," Masika alisema.Mwimbaji huyo wa kibao 'Mwema' alisema kwamba mkutano wa kwanza na mumewe ilikuwa ya kawaida tu. Wawili hao waliendelea kuchumbiana kwa miezi kadhaa kabla ya kufunga pingu za maisha hatimaye."Nilikuwa na nia ya maombi yangu. Tulifunga ndoa, ilikuwa nzuri na sasa tuna watoto watatu. Tuko hapa sasa," alisema.Masika alisema walichumbiana sana na mumewe na kuzungumza mengi kabla ya kuchukua hatua ya kufanya harusi. Alibainisha kuwa maisha yake ya maombi yamechangia pakubwa kufanikisha ndoa yake.Mwanamuziki huyo alifichua kwamba alipata mpenzi wake wa kwanza akiwa katika chuo kikuu cha Daystar ila mahusiano hayo hayakudumu."Alikuwa mtu mcha Mungu sana. Alikuwa akinifundisha neno la Mungu. Lakini haikufanya kazi," alisema.Aliendelea kujaribu mahusiano na wacha Mungu wengine katika chuo kikuu ila hakuna ambayo yalidumu. Alisema hatimaye alikutana na Bw David mwaka ambao alikuwa akihitimu na wakafunga ndoa mwaka moja baadaye.Katika mahojiano ya awali, Masika alifichua kwamba alikutana na mwenzi wake wa maisha alipokuwa akitumbuiza kwenye karamu ya harusi katika eneo la Lang'ata ambapo Muguro alikuwa mpiga video."Aliomba nambari yangu baada ya tukio akipendekeza kwamba angependa niimbe kwenye harusi yake siku moja," alisema.Alisema alijua David angekuwa mumewe punde baada ya kukutana naye mara ya kwanza.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni

MUACHE KUNIA BUDU MIMI SIO YESU

ROBERT POWELL MUIGIZAJI WA FILAMU YA YESU AMEWAAMBIA WAKRISTO   "MIMI SIYO YESU, ACHENI KUNIABUDU"  Mwigizaji Robert P...